Y

YouLibs

Remove Touch Overlay

Salama Na BARBARA HASSAN SE6 EP14 |MORNING GLORY PART 1|SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Duration: 24:58Views: 35.7KLikes: 332Date Created: Apr, 2022

Channel: YahStoneTown

Category: Entertainment

Tags: marcochalimwanafasalamajabirgigy moneymxcartergigi moneysalamanaayyah stonetown yahstonetownjokatekhadijakopadiamondplatnumzfidq

Description: #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460 MORNING GLORY Barbara Hassan’s voice is ICONIC, imebidi nianze kwa kuandika kizungu ili ikae pale ninapotaka mimi, si unakumbuka walikua wakisema kwa kuonyesha msisitizo mmoja inabidi aongee Kingereza na hilo ndo nlilojaribu kufanya hapo. Amekua consistent kwa miaka zaidi ya kumi, mida yake ya kuamka ni ile ile na ya kulala pengine hubadilika kutokana tu na mood yake. Ukiachana na sauti tamu ambayo itakufanya usione hatari kama umeamka alfajiri, Bi Barbara pia ana lafdhi tamu ya ki pwani, maneno yanatamkwa yapasavyo kabisa kitu ambacho huwezi kukiwekea dhamana kwa watangazaji wa skuizi ambao asilimia kubwa si waongeaji wa Kiswahili fasaha na matamshi pia hawayawezi. Wengi wana shida za R na L na hawaana habari! Kabila lake ni Mchaga na mimi ni moja kati ya watu ambao tulikua tunadhani Barbara si Mtanzania, ila alikulia zake Kenya huko na huko ndo accent yake nzuri inayomfanya yeye awe yeye ilikotokea. Aliniambia kwenye kipindi kwamba miaka ya hivi karibuni amakua akiskia watu wengine wakiongea kama yeye kwenye vyombo vya habari na akasema pia si kama inamchukiza ila anataka tu watu wawe WAO na si kuinga mtu mwengine maana huyu tayari yupo. Barbara amekua kwenye POWER BREAKFAST kwa miaka mingi, na kwa mujibu wake wengi wamekuja wakaenda na wakarudi na yeye amekua pale pale kama JABALI, hakutetereka kwenye kipindi ambacho watangazaji wengi mahodari walikua wanahama Radio moja kwenda nyengine kwa dau KUBWA la ada ya uhamisho na mishahara mara dufu ya waliyokua wanalipwa ila yeye alisimama imara ingawa offer zilikua zinakuja mezani, moja kwa moja kwake na nyengine kwa kutumia watu wake wa karibu. Humu Bi Barbara anatuhadithia jinsi alivyoenda kuomba kazi kwa mara ya kwanza, yeye hakua na mtu wa kumshika mkono au wa kumumbia fanya hili na lile, anasema akiwa mbichi kabisa baada ya kumaliza shule alienda zake pale Clouds FM enzi hizo Radio iko jengo la Kitega Uchumi na kumuomba mlinzi kwamba anataka kuonana na Bosi, mlinzi nae hakua na hiyana maana Boss alikuwepo ila alimuuliza tu kama ana miadi na yeye wala hakumdanganya, alikuambia miadi hana ila ilikua MUHIMU kwa yeye kuonana nae. Na nafasi ya kuonana na Boss Ruge ikapatikana. Barbara anakumbuka maongezi yao kama ilikua jana, na kwake yeye Marehemu Ruge Mutahaba ni kama Robin Hood kwa jinsi alivyokua akiyaishi maisha yake. Nisingependa nikueleze meeengi ambayo mimi na Rafiki yangu huyu tuliyaongea ila kwa faida yako ningependa sana uskilize maswali na majibu yake kwa urefu ili twende sawa. Oh pia nilikua sijamuona binti yake Ashley toka kazaliwa lakini nilipata bahati ya kukutana naye alipokuja kwenye set ya maongezi haya. Yangu matumaini kama kawaida utaokota mawili matatu ambayo yatakusaidia kwenye maisha yako. Tafadhali enjoy and Happy Holidays. Love, Salama. Support us through anchor.fm/yahstonetown/support SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs Listen our Podcast on Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬ ‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬ GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack ‪YouTube Link bit.ly/YoutubeSalamaNa Soundtrack Yeah by @MarcoChali youtube.com/watch?v=Cue1HB4fnLQ Follow: Twitter: twitter.com/YahStoneTown Instagram: Instagram.com/YahStoneTown Facebook: facebook.com/YahStoneTown Channel Administered by Slide Digital Instagram: instagram.com/slidedigitaltz

Swipe Gestures On Overlay